Zitto Ataka Hatua Kali Zichukuliwe Dhidi ya Askari Polisi Aliyemtishia Bunduki Adam Malima
Katika hali isiyokuwa ya kawaida iliyotokea jana Jijini Dar es salaam kwa kitendo cha aliyekuwa Naibu Waziri Wizara ya Fedha katika utawala wa awamu ya nne, Adam Malima kutishiwa bunduki na askali mmoja aliyekuwa doria kimewashangaza wengi na kupelekea Mbunge wa Kigoma Mjini, Zuberi Zitto Kabwe kuonyesha masikitiko yake hadharani kwa kitendo kilichofanywa na askali huyo.
Zitto kabwe ameonyesha masikitiko hayo kupitia ukurasa wake wa kijamii Facebook akihoji kama polisi wanafundishwa kuwafanyia hivyo raia wasiokuwa na hatia kiasi cha kuibua hofu katika jamii inayowazunguka na kupoteza imani na jeshi hilo la polisi.
“Hii ni nini ?, askari wetu wanafundishwa kufanya hivi, Waziri Mwigulu huyu yupo wazi na ni wa kutoka kwako. Unahitaji uchunguzi”. Ameandika Zitto.
Zitto aliandika hayo baada ya muda mchache kupita kwa tukio hilo
lililowahusisha askari hao walioambatana na kampuni ya Majembe Auction
Mart waliokuwa wakitaka kujaribu kukamata gari iliyokuwa imeegeshwa
pembeni ya barabara ya Masaki karibu na Hoteli ya Double tree ingawa
ndani ya gari hilo alikuwepo dereva.
No comments