Said Mecki Sadiki Ataja Sababu Zilizomfanya Aandike Barua Ya Kuacha Kazi ya Ukuu wa Mkoa
Aliyekuwa Muu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecki Sadiki , amesema ameamua kuondoka serikalini baada ya utumishi wa muda mrefu na anakwenda kupumzika mkoani Mwanza huku akiwa mfugaji wa samaki.
Aidha
Sadiki alisema pia kulingana na afya yake, anahitaji kupisha vijana
wadogo wamsaidie Rais Dk John Pombe Magufuli kulingana na kasi yake
kwani yeye ameepuka kumkwaza rais wakati wa utekelezaji wa majukumu yake
kama mkuu wa mkoa.
“Uamuzi
huu wa kupumzika nilimuomba rais kwa muda mrefu sana, na nikirudi
kijijini nitaendelea na ufugaji Samaki maana nilishaandaa bwawa la
kufugia, nitaendelea nalo huku nikiwaza jambo lingine la kufanya,” alisema.
Sadiki
alisema hayo jana wakati akitaja sababu zilizochangia kumuomba Rais
Magufuli kuacha kazi yake ya ukuu wa mkoa wa Kilimanjaro.
“Namshukuru
rais kuridhia ombi langu, nimetumikia serikali tangu mwaka 1999 nikiwa
mkuu wa wilaya na baadaye mkuu wa mkoa kuanzia mwaka 2005 hadi sasa
ninapoondoka mwenyewe... nimeona ni wakati muafaka kumweleza aliyeniteua
kuwa nahitaji kupumzika nikiwa na akili timamu na afya njema,” alisema.
Alisema
Sababu nyingine kubwa ni kuhofia afya yake kutomudu kasi ya rais
Magufuli, kwani alifanywa upasuaji mwaka 2012 na 2014 nchini India
ingawa hakutaka kuweka wazi maradhi yaliyokuwa yakimkabili.
“Kama
kiongozi muungwana lazma ifike mahali ukiri kwamba wapo vijana wenye
uwezo mzuri na kasi ambayo inaendana na serikali ya awamu ya tano...
mimi nilishatekeleza wajibu wangu na mchango kwa serikali yangu, sasa
inatosha, tupate mawazo na michango ya wengine,” alisema.
Sadiki
ambaye amekuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro tangu Machi 13,2016
alipoteuliwa na Rais Magufuli, alisema siyo vibaya kwa kiongozi
kujitathmini na kuwaachia wengine kama atabaini kasi yake ya utendaji
kazi imeanza kupungua.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,
Ikulu, Gerson Msigwa, mkuu wa mkoa Sadiki pamoja na aliyekuwa jaji wa
Mahakama Kuu ya Tanzania na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebeisha Sheria
Tanzania, Aloysius Mujulizi na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Upendo
Msuya waliomba kuacha kazi na rais akaridhia
No comments