Bibi kizee apandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuiba gari
Fatuma Mohammed (70) na Aziz Njakula (36) wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya wizi na kupatikana na gari la wizi aina ya Toyota Hiace.
Wakili wa Serikali, Hamisi Said, amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa Julai 9, 2015 eneo la Mnazi Mmoja walitenda kosa la wizi wa gari hilo mali ya kampuni ya Choice Motors.
Januari 26, 2016 eneo la Nzasa, Dar es Salaam, Bi Fatuma anadaiwa alikutwa akiwa na gari la wizi nyumbani kwake. Baada ya kusomewa mashtaka washtakiwa wamekana na upande wa Jamhuri ulidai upelelezi haujakamilika.
Hakimu Simba ametoa masharti ya dhamana kwamba wawe na wadhamini wawili kila mmoja ambao watasaini bondi ya Shilingi milioni 10. Ambapo Walikamilisha masharti na kuachiwa kwa dhamana.
No comments