MAGARI YA KIFAHARI YATAWALA MSIBA WA BILIONEA IVAN SSEMWANGA
Magari ya kifahari yameonekana jana 
katika mazishi ya bilionea Ivan Ssemwanga yaliyofanyika nyumbani kwao 
Kayunga jijini Kampala nchini Uganda.
Ivan aliyekuwa mume wa Zari Hassan 
maarufu ‘Zarithebosslady’ ambaye kwa sasa ni mpenzi wa Diamond Platnumz,
 alifariki dunia wiki iliyopita baada ya kupata kiharusi na kuwa katika 
hali ya koma kwa wiki mbili mfululizo katika hospitali ya Steven Biko 
huko Pretoria nchini Afrika Kusini.
Gazeti la Uganda, Daily monitor 
linaripoti kuwa miongoni mwa magari hayo ni pamoja na yale ya marehemu 
likiwemo Hammer lenye jina la Ivan 9, yale ya vizito mbalimbali wa jiji 
la Kampala waliohudhuria mazishi hayo pamoja na gari la tajiri wa 
Tanzania Jack Pemba aina ya Audi lenye jina la A Pemba ambalo 
lilionekana kuwa la kifahari zaidi.
Katika hali ambayo haikuonekana kuwa ya 
kushangaza, baadhi ya waombolezaji walionekana wakiomba na kupewa fedha 
kutoka kwa matajiri mbalimbali waliohudhuria.
Hata hivyo kaburi la Ivan liliwekwa mafungu ya fedha chini ikiwa ni maandalizi ya kuuweka mwili wa bilionea huyo.
Mwili wa Ivan ambao uliwasili Uganda 
siku mbili zilizopita katika ndege kubwa iliyobeba watu 50, umezikwa 
katika makaburi ya familia pembeni ya kaburi la baba yake.
Chanzo - Mwananchi

No comments