Breaking News

Hifadhi ya Ngorongoro ni noma! – Nay wa Mitego

Msanii wa muziki wa hip hop, Nay wa Mitego ametembelea hifadhi ya wanyama ya Ngorongoro iliyopo mkoani Arusha, na kujionea ufahari wa mbuga hiyo.

Akizungumza na Bongo5, Nay amedai ni mara yake ya kwanza kutembelea hifadhi hiyo na kujionea wanyama mbalimbali pamoja na kupata mafunzo na historia.
“Hakuna siku nime-enjoy kama siku ya Jumatatu nilipotembelea mbuga za wanyama za Ngorongoro. Mimi na team yangu nzima, tumejifunza vingi ambavyo Watanzania wengi tunatakiwa kuvijua kuhusu mbuga zetu na raha ya kutalii wenyewe kama wazawa kwenye mbuga zetu. Wazungu sio wajinga kufunga safari toka Ulaya kuja kuona wanyama Ngorongoro Crater ni raha sanaa,” alisena Nay.
“Nimejua zaidi kuhusu Simba na tabia zake nyingi ambazo wengi hatuzijui. Tena nimegundua tukiwa pale wanajisikia raha kwa sababu ni kama tunacheza nao. Pia nimegundua kuna tofauti ya wanyama wa mbuga ya Ngorongoro na mbuga zingine,” alisema Nay wa Mitego. Aliongeza,
Rapa huyo amedai kwa sasa atakuwa anaweka utaratibu kila mwaka wa kutembelea mbuga mbalimbali za wanyama akiwa na familia yake.

No comments