Mkubwa Fella hamsaidii msanii anayefanya kazi zake binafsi.- Aslay
Mkurugenzi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Saidi Fella maarufu pia kama Mkubwa Fella amekosolewa hadharani na Aslay.
Akiongea katika kipindi cha Zero Planet cha Ice Fm, Aslay alisema kuwa Mkubwa hamsaidii msanii anayefanya kazi zake binafsi.
“Ni kweli Mkubwa yeye anasimamia Yamoto Band, Mkubwa hasimamii msanii mmoja mmoja, kwahiyo unatakiwa ufanye kitu cha ziada ilimradi ngoma zako zifike. Wenzangu wanaandaa vitu vinakuja lakini mimi nimefanya kama kuwaonesha njia,”Aslay alisema.
Aliyosema Aslay yanapinga maneno ya Mkubwa Fella aliyosema hapo nyuma kuhusu kusupport wasanii wa Yamoto Bend wanaofanya miradi yao binafsi.
No comments