Kundi Jipya la wasanii wa Hip Hop Bongo SSK lifahamu zaidi hapa.

SSK ni kundi jipya la Hip Hop linaloundwa na Wakazi, Zaiid, P The MC na Cjamoker (Producer).
 Muunganiko wa emcees hawa wenye ladha tofauti nao umeweza kuzaa kitu 
tofauti ambacho hakijazoeleka kutoka kwao wakiwa wanafanya kazi as solo 
artists.
Wakizoeleka kama punchline rappers, SSK kwa ujumla wamefanikiwa 
kubadilisha dhana hiyo na kuweza kufanya Muziki ambao unalenga mambo ya 
kijamii hususan Mahusiano, Uchumi, Furaha, Imani na Mapito ya maisha na 
kadhalika, na wamefanikiwa kufanya hivyo kwa kutumia lugha nyepesi na 
bado kwa kuzingatia misingi ya Muziki wa Hip Hop. SSK inatarajia 
kuwaonesha mashabiki upande wa pili wa rappers hawa ila pia kuwa funzo 
la umoja, hususan katika kipindi hiki ambacho makundi na umoja wa 
Wasanii unavunjika kila siku.
Jina la SISI SIO KUNDI lilikuja kiutani ila lina maana kwa sababu, kila 
msanii ataendelea kuwa na individual brand ila umoja unakuja pale 
wanapofanya kazi kama SSK. Ila pia sisi sio kundi sababu ni zaidi ya 
kundi, maana malengo yetu tunayotarajia kuyafikia ni kuwa zaidi ya kundi
 la muziki.
Kundi lilizaliwa wakati wa utayarishaji wa wimbo wa “Cjamoker” ambao 
marapper wote hawa walishiriki. Wimbo rasmi wa utambulisho wa kundi 
unaitwa “Habari Ya Leo” na tayari SSK wapo kwenye hatua za mwisho Za 
uandaaji wa Album yao itakayoitwa “SISI SIO KUNDI”. Mabibi na Mabwana 
nawaletea kwenu… SSK!! @ssk_tanzania @chimbo_inc #workethic #BigMoyo 
@instincts_records #ChamaLaVita #SSK #SisiSioKundi
No comments