Breaking News

Picha: Zari atua hospitali kumjulia hali ex wake Ivan

Mama watoto wa Diamond, Zari the Bosslady ameonekana katika picha akimjulia hali ex wake Ivan Ssemwanga ambaye anadaiwa kulazwa katika hospitali moja nchini Afrika Kusini baada ya kupata matatizo ya moyo.

Zari akiwa hospital kumjulia hali ex wake

Ivan ambaye alipata watoto watatu na Zari, anadaiwa kukimbizwa hospitali wiki hii baada ya kupoteza fahamu.

Jumatatu hii Zari alipost picha ya mshumaha na kuwaomba mashabiki wake kumuombea mzazi mwenzake huyo.

Hapo jana Zari kupitia ukurasa wake wa SnapChat aliandika “Siku mbili kwangu zimekuwa ngumu, nawaomba tumuombee Ivan”.

Mitandao ya Uganda inadai kuwa Ivan anasumbuliwa na maradhi ya Shambulio la Moyo (Coronary Artery Disease).

No comments