TANZANIA YAKUBALI KUPELEKA WALIMU WA SOMO LA KISWAHILI RWANDA
Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli amepokea barua yenye ujumbe wa Rais
wa Jamhuri wa Rwanda Mhe. Paul Kagame iliyowasilishwa kwake na Mjumbe
Maalum ambaye ni Waziri wa Elimu wa Rwanda Dkt. Musafiri Papias Malimba.
Pamoja na kupokea barua hiyo, Mhe. Rais Magufuli na Dkt. Musafiri Papias
Malimba wamezungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya
Tanzania na Rwanda ikiwemo katika sekta ya elimu hususani maendeleo ya
sayansi na teknolojia.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameipongeza Rwanda kwa kuamua lugha ya
Kiswahili ianze kufundishwa katika shule zake na ameahidi kuwa Tanzania
ipo tayari kutoa walimu wa kwenda kufundisha lugha hiyo.
No comments