TBL YAZINDUA KAMPENI YA ‘CASTLE LITE UNLOCKS’ JIJINI DAR ES SALAAM.
 Meneja Masoko wa 
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),  Idara ya Kuunganisha Wateja Afrika 
Mashariki, George Kavishe (kulia), akizungumza na waandishi wa habari 
Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa kampeni
 ijulikanayo, ‘Castle Lite Unlocks’. Kushoto ni Meneja Chapa Msaidizi wa
 Bia Laini Tanzania, Isaria Kilewo na katikati ni Meneja Masoko wa TBL Kitengo cha Bia Laini Afrika Mashariki, Amou Majok.
 Meneja Masoko wa TBL Kitengo cha Bia Laini Afrika Mashariki, Amou Majok (katikati), akizungumza kwenye mkutano huo.
 Mkutano ukiendelea.
 Waandishi wa habari wakiwa katika uzinduzi huo.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
 Wadau wakibadilishana mawazo katika mkutano huo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya kutengeneza Bia  Tanzania 
(TBL)) leo imezindua kampeni ijulikanayo, ‘Castle Lite Unlocks’ ambayo 
lengo lake ni kuhamasisha wateja wake wa bia chapa Castle Lite 
kuifurahia zaidi na pia kuwaleta pamoja katika tamasha kubwa 
litalofanyika mwezi wa Julai mwaka huu.
Akizungumza katika mkutano na waandishi 
wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa hafla ya uzinduzi wa 
kampeni hiyo uliofanyika katika ofisi za TBL zilizoko Masaki, Meneja 
Masoko wa TBL Idara ya Kuunganisha Wateja Afrika Mashariki, George 
Kavishe, alisema TBL kwa miaka imekuwa ikijikita katika kuwafurahisha na
 kuwachangamsha wateja wake, hasa vijana kwa matamasha ikiwemo muziki 
ambao upo katika vipaumbele vya kampuni hiyo.   
“Uzinduzi huu utafikia kilele chake 
tarehe 22 mwezi wa Julai mwaka huu ambapo kutakuwa na tamasha kubwa Dar 
es Salaam litakalowapa nafasi wateja wetu kushuhudia wanamuziki wakubwa 
wa ndani na nje ya nchi, hivyo kuwapa wateja burudani itakayokuwa kwenye
 kumbukumbu zao kwa muda mrefu”, alisema Kavishe.   
Kavishe aliongeza kuwa kwa kipindi hicho
 cha miezi mitatu ya kampeni, zawadi kedekede zitatolewa zikiwemo muda 
wa maongezi wa simu za mkononi wa zaidi ya milioni 30 na pia tiketi 
zaidi ya elfu moja kwa washindi wa droo ambazo zitakuwa 
zinashindanishwa.
Aliongeza kwamba bajeti ya kampeni nzima ni zaidi ya shilingi milioni mia saba.
Naye Meneja Masoko wa TBL Kitengo cha 
Bia Laini Afrika Mashariki, Amou Majok alisema kuwa TBL ina utaratibu 
mahsusi wa kuandaa matamasha mara kwa mara ili kuwashukuru wateja wake 
kwa kuwapa burudani na kuwahamasisha kuzifurahia vinywaji vyake ambavyo 
ni vya hali ya juu na vyenye ubora zaidi.   
No comments