MENEJA WA MSHAMBULIAJI KINDA WA SIMBA ALIA NA KOCHA OMOG
Meneja
 wa kiungo mshambualiaji wa Simba, Hija Uganda amelalama kwamba kitendo 
cha Kocha Joseph Omog kutompa nafasi ya kucheza mchezaji wake ni kuua 
kipaji chake.
Meneja
 wa Ugando, Jamali Kisongo amesema kuwa kitendo cha mchezaji huyo kukosa
 nafasi ya kucheza chini ya Omog, kimekuwa hakimfurahishi ndipo 
alipoamua kuchukua uamuzi huo wa kutaka aondoke zake klabu hapo ili 
akatafute maisha sehemu nyingine ambako atakuwa akipata nafasi ya 
kucheza mara kwa mara.
“Kwa
 mchezaji anayejitambua hata siku moja hafurahii kukaa benchi bila ya 
kucheza, Ugando kwa sasa maisha yake ndani ya Simba siyo mazuri hapati 
nafasi ya kucheza jambo ambalo linaweza kuua kipaji chake.
“Kutokana
 na hali hiyo, hivi sasa nipo katika mazungumzo na uongozi wa Simba ili 
baada ya msimu huu uweze kumuachia akatafute maisha sehemu nyingine 
ambako atapata nafasi ya kucheza ili aweze kuinua kipaji chake,” alisema
 Kisongo.

No comments