Breaking News

Aliyemuua babu yake mbeya na kumtundika mtini ili kurithi ng'ombe kunyongwa hadi kufa.

Image result for kitanzi

Baada ya kumuua babu yake akitaka kurithi ng’ombe kwa nguvu, Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya imemhukumu kunyongwa hadi kufa mkazi wa Kijiji cha Sakamwela wilayani Mbozi, Geofrey Sichizya.Mahaka hiyo imentia hatiani Sichizya kwa kumuua babu yake kwa kukusudia ili kujipatia ng’ombe tisa wa mzee huyo.

Hukumu hiyo ilisomwa juzi na Mahakama hiyo iliyohamishia vikao vyake katika Mahakama ya Wilaya ya Mbozi.Jaji Atuganile Ngwala alisema baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili Mahakama imeridhika pasipo kuwa na shaka kwamba,mshtakiwa alimuua babu yake,Labson Sichizya kwa kukusudia akiwa na lengo la kujipatia ng’ombe.

Alisema ushahidi uliotolewa na mashahidi watatu ambao ni ndugu wa mshtakiwa akiwamo baba yake mzazi, Meas Sichizya; Mashaka  na Sikitu Sichizya pamoja na maelezo binafsi ya mshtakiwa umethibitisha pasipo kuacha shaka kuwa alitenda kosa hilo.Jaji Ngwala alisema ndugu wa mshtakiwa waliithibitishia Mahakama kwamba wao ndio waliomkamata kwa kushirikiana na mwenyekiti wa kijiji na kumpeleka kituo cha polisi.Katika maelezo ya mshtakiwa aliyoyatoa mbele ya mlinzi wa amani, alisema yaliithibitishia Mahakama kwamba alitenda kosa hilo.

Jaji Ngwala alisema mshtakiwa katika maelezo hayo alidai alichukua uamuzi wa kumuua babu yake ili kuchukua na kumiliki ng’ombe aliokuwa akiwafuga.Alisema  baada ya mshtakiwa kumuua babu yake aliufunga shingoni mwili wake kwa kamba ya chandarua na kumning’iniza kwenye mti nyuma  ya nyumba yake ili ionekane kuwa alijinyonga.


No comments