WATU WANAODAIWA KUWA WAPENZI WAMEUAWA KWA KUCHOMWA MOTO JUU YA GODORO ARUSHA
Watu
wawili wanaodhaniwa ni wapenzi, wameuawa kwa kuchomwa moto baada ya
kufungwa kamba wakiwa kitandani, katika tukio lililotokea eneo la
Whiterose lililoko kata ya Kiranyi wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Mamia
ya watu wamejitokeza kuzunguka nyumba lilipotokea tukio hilo baada ya
kuona moshi ukitoka katika moja ya chumba na kuonekana miili ikiwa
imeteketea kwa moto.
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,Charles Mkumbo amesema tuki hilo limetoke jana, Jumanne saa 3.00 asubuhi.
Amesema
aliyekutwa amefariki ni Maurine Urio (32) pamoja na rafiki yake huyo
ambaye hajaweza kutambulika kutokana na kuungua sana.
“Tumepata
taarifa asubuhi hii kuwa kuna nyumba inaungua na polisi pamoja na
zimamoto walifika eneo la tukio na kukuta watu hao wameshapoteza maisha
wakiwa juu ya godoro ambako mwanaume alionekana kabla ya kuchomwa
alifungwa kamba miguu na mikono ili kuzibitiwa,”amesema.
Mkumbo
amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia
maiti katika hospitali ya mkoa Mount Meru huku wahusika wa tukio hilo
wakiwa wanatafutwa.
Akizungumzia
tukio hilo mwenyekiti wa mtaa wa Ilkiurei iliyoko kata ya Kiranyi,
Onesphory Chami amedai kuwa tukio hilo linahusishwa na wivu wa mapenzi.
No comments