Breaking News

Picha: Vanessa kufanya kolabo na kundi la Major Lazer la Marekani?

Msanii wa muziki kutoka Tanzania, Vanessa Mdee amekuwa miongoni mwa mastaa waliohudhuria tuzo kubwa za muziki za chati za Billboard nchini Marekani.

Vanessa akiwa na Diplo
Tuzo hizi zinatolewa na kampuni inayosimamia chati za muziki wote duniani, na hutolewa kwa vigezo vya wimbo kuwa na redio na TV play kubwa, mauzo ya albumu na single, mauzo ya mtandaoni na streaming na umaarufu mtandaoni kwa mwaka huo.
Usiku huo Vanessa aliweza kukutana na wadau mbalimbali wa muziki akiwemo, Diplo mmoja kati ya wasanii wanaounda kundi kubwa la muziki liitwalo Major Lazer la nchini Marekani.
Muimbaji huyo alipost video fupi akiwa na staa huyo na kuandika “Wait for that Major Lazer x VeeMoney 🇹🇿 x 🇺🇸#billboardmusicawards,”

Diplo

Vanessa Mdee

No comments