Nikki wa Pili amemchana Lord Eyez kwa kumwambia sio kweli kwamba Weusi wanaubinafsi
Msanii wa 'Hip hop' na msemaji wa kampuni ya Weusi, Nikki wa Pili amemchana Lord Eyez kwa kumwambia sio kweli kwamba wanaubinafsi kama yeye anavyodai huku akisema laiti wangekuwa wabinafsi basi wasingeweza kuwa hata marafiki baina yao.
Niki amebainisha hayo kupitia kipindi cha FNL kutoka EATV baada ya msanii Lord Eyez kudai kuwa kundi hilo wanaubinfasi na unafki ndiyo maana ameshindwa kuendelea kufanya nao kazi na kuamua kutoka katika umoja huo kwenda kusimamiwa kazi zake za kimuziki na Baraka De Prince.
"Bonta na Joh Makini urafiki wao unazaidi ya miaka 15, mimi na G Nako tuna urafiki zaidi ya miaka 12 'so' watu wenye ubinafsi hawawezi kuwa marafiki kwa 'fact' hiyo ndogo unaweza ukapima....Sio kweli kwamba wasanii wa kundi hupeana ushirikiano kwenye kazi na 'issue' zingine na mtu wa kulalamika hivyo alipaswa kuwa Bonta ambaye amekuwa nje ya kundi kwa muda kidogo ila sio Lord". Alisema Nikki wa Pili
Pamoja na hayo, Niki alibainisha baadhi ya mambo kwa kusema kampuni haina ugomvi na Lord Eyez muda wowote akikamilisha masharti alioambiwa anaweza kukaribishwa tena upya kufanya kazi na kundi hilo la weusi kutoka Arusha.
"Lord Eyez na kampuni wapo vizuri nafikiri kampuni ilishampa A,B,C zake yeye mwenyewe tu akizikamilisha tu hakuna tatizo". Alisisitizia Nikki wa Pili
No comments