Nedy Music ataja kosa lake analijutia kwenye muziki
Nedy Music amefunguka kosa ambalo amekuwa akilifanya kwenye muziki na ambalo analijutia.
Muimbaji huyo amekimbia kipindi cha The Playlist cha Times FM, “Zamani nilikuwa na mchezo nikikaaga naandika nyimbo moja kama hivi nikija nikiitambulisha kama hivi ‘Dozee’ siingii studio mpaka Dozee nikiona kabisa mwisho wake, na kama inahitajika ngoma mpya ndo narudi tena studio.”
“Sio kitu kizuri kwangu, hicho nilichokua nafanya, sasa hivi, huku Dozee ipo lakini naendelea kupika studio ngoma kali ambazo naamini kwamba hata nikipachikia pachika watu wana enjoy good music,” ameongeza.
Kwa sasa msanii huyo anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Dozee’ aliouachia wiki iliyopita.
No comments