Manusura wa Lucky Vicent aliyefanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo aonyesha dalili njema.
Manusura
wa ajali ya Lucky Vincent, Doreen Mshana, amepata hisia katika miguu
yake yote miwili, ikiwa ni siku chache tangu afanyiwe upasuaji mkubwa wa
uti wa mgongo.Hiyo ni ishara kuwa upasuaji mkubwa wa uti wa mgongo
aliofanyiwa, umefanikiwa.
Wenzake
Wilson Tarimo na Saidia Ismael wameruhusiwa baada ya kupata matibabu na
sasa wanaendelea na mazoezi ya viungo katika nyumba maalum kwa wagonjwa
waliovunjika viungo jijini Sioux.Walikuwa wamelazwa katika Hospital ya
Mercy Sioux City, Marekani walikokuwa wakipata matibabu baada ya ajali
mbaya ya basi iliyoua wanafunzi wenzao 32, Mei 6 mwaka huu.
Mbunge
wa Singida Kaskazini(CCM) Lazaro Nyalandu, amesema Doreen ameweza
kuisogeza miguu yake miwili kwa mara ya kwanza tangu apate ajali
hiyo.“Tuendelee kumuombea,huu ni uponyaji wa uti wake wa mgongo.”
amesema Nyalandu katika mtandao wake wa facebook.Pia watoto Saidia na
Wilson, pamoja na wazazi wao, walikwenda Hospitali kumuangalia Doreen
leo ambaye bado amelazwa akiendelea na matibabu.
No comments