KESI YA WEMA SEPETU KUTUMIA BANGI YAPIGWA KALENDA
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini
Dar es Salaam, imeambiwa kwamba upelelezi wa kesi ya kukutwa na bangi
inayomkabili Muigizaji maarufu, Wema Sepetu na wenzake umekamilika.
Hatua hiyo imefikiwa ambapo upande wa
Jamhuri mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alisema kwamba
upelelezi umekamilika dhidi ya msanii huyo na wakili wa Serikali Helleni
Mushi aliomba kesi hiyo kuarishwa na kupangwa tarehe ya kuanza
kusikilizwa ili watuhumiwa waanze kusomewa maelezo ya awali.
Katika kesi ya msingi, Wema anatuhumiwa
kukutwa na msokoto mmoja wa bangi na vipande viwili vidogo vya bangi
vyenye uzito wa gramu 1.08.
Mbali na Wema washitakiwa wengine ni
wafanyakazi wake wa ndani Angelina Msigwa (21) na Matrida Abas (16),
ambapo wote wanashtakiwa kwa kosa moja la kukutwa na kiasi hicho cha
dawa za kulevya.
Inadaiwa kuwa Wema na wenzake walitenda
kosa hilo Februari 4 mwaka huu, nyumbani kwao Kunduchi Ununio , Wilaya
ya Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam.
Hakimu Simba alisema kesi hiyo itaanza kusikilizwa, Juni Mosi, mwaka kwa watuhumiwa kuanza kusomewa maelezo ya awali.
No comments