G Nako afunguka habari za kuhusishwa na 'wizi'
Rappa kutoka kundi la Weusi G Nako mwenye 'hit song' ya 'Ma Ole' amefunguka kuhusu tuhuma za kushiriki katika ngoma za wizi kwa kukanusha kwamba hajawahi kufanya hivyo hata siku moja japokuwa ala za muziki mara nyingi huwa zinafanana.
G Nako amelazimika kufunguka hayo baada ya kuhusishwa katika tuhuma za ku-'copy' na ku-'paste' nyimbo mbili kutoka kwa wasanii tofauti tofauti ambazo ni 'Go low' walioshirikiana na Jux ikielezwa kwamba ameiba 'chorus' kutoka Nigeria pamoja na 'Ma ole' ambayo wameshirikiana na Belle 9 nayo akaibuka Tox Star kutoka bongo na kudai kuwa 'melody' ya wimbo huo umeibwa kutoka katika wimbo wake wa 'Ole' alioufanya miaka miwili iliyopita.
"Mimi napokuwa studio huwa sifikirii kitu kutoka kwa mtu mwingine yoyote na mara nyingi napokuwa nafanya kazi zangu studio nakuwa nipo 'in my zone', nakuwa kwenye hisia zangu mwenyewe za tofauti kwa hivyo inakuwa ni ngumu sana kukuta kitu changu nilichofanya kinafanana na mtu mwingine. Kinaweza kikawa kinafanana kinamna labda 'melody' za kimuziki lakini hakiwezi kikawa kimefanana 'hundred percent' kwa sababu mara nyingi utakuta 'code' za muziki zinaingiliana. Ni vitu vya kawaida kwenye muziki lakini sijawahi kufanya kitu ku-compare na mtu mwingine sijawahi kufanya kitu kwa sababu nimemsikia mtu mwingine" alisema G Nako kupitia eNewz ya EATV.
Pamoja na hayo, G Nako amesema hakuna chochote kinachomuathiri katika utendaji kazi wake wa kimuziki kutokana na watu kudai ana-copy kazi za wasanii wengine waliokwisha kufanya kabla yake.
No comments