Amber Lulu sasa atangaza kutoa ajira rasmi
Msanii wa bongo fleva mwenye 'hit song' ya 'Watakoma' Amber Lulu amefunguka kwa kusema sasa hivi hatajishughulisha tena na masuala ya 'video queen' na badala yake atafungua kufungua kampuni yake ya 'video vixen' hivi karibuni.
Amber Lulu amebainisha hayo baada ya kusumbuliwa na wasanii wengi katika simu wakimuhitaji aende kuwafanya kazi yake aliyokuwa anaifanya hapo awali ya unenguaji katika muziki kabla ya kuamua kuingia rasmi katika kuimba huku wengine wakimtaka awatafutie warembo kwa ajili ya kazi hiyo.
"Mimi sifanyi hivyo vitu tena, mimi sasa hivi ni msanii kwa hiyo siwezi kurudi nyuma, sasa hivi natakiwa niwaite ma-video vixen ambao watakuwa kwenye ngoma zangu. Mimi ni boss wa ma- video queen na soon nafungua kampuni yangu ambayo itakuwa inajishughulisha na warembo na wapo tayari wakali 10" alisema Amber Lulu.
No comments