Breaking News

“Tulimpunguza Baraka” Ben Pol aeleza chanzo cha bifu yake na Baraka The Prince


“Tulimpunguza Baraka” Ben Pol aeleza chanzo cha bifu yake na Baraka The Prince
Baraka the Prince ana bifu kubwa na Ben Pol na Jux. Ben Pol ameeleza chanzo cha kilochosababisha wao kutoelewana na walikua marafiki awali.
Ben Pol and Baraka wamewai kushirikiana kuachia wimbo unaoitwa ‘Mwambie’. Hata hivyo wiki mbili zilizopita Baraka alimkashifu Ben Pol alipowachia wimbo wake mpya ‘Tatu’.

Baraka the Prince na Ben Pol
Ben Pol sasa ameeleza nini ilitokea kati yake na Baraka the Prince; katika mahojiano na Ayo TV, Ben Pol alisema Baraka alianza kuwa na chuki nay eye na Jux baada ya wao kumpuguza kimuziki kwa kushirikiana kufanya shows pamoja na tours.
“Mimi napenda sana kukoselewa, napenda kupokea maoni lakini ina matter sana maoni yanatoka kwa mtu gani au wewe na huyu mtu mko kwenye situation gani. Baraka maoni yake yanaweza yakawa mazuri, yanaweza yakawa ni ya kuboresha, yanaweza yakawa ya kujenga, kukosoa. Lakini mimi nawaza status yangu na Baraka ilivyo sasa sahi alafu nahusianisha na yale maoni yake, naona kuna msuguano. Baraka ana hali ya chuki na mimi, especially mimi na Jux, wote wawili sisi ana matatizo na sisi, ana chuki. Ata last time tulikutana naye alikua hataki kutusalamia akageuza mgongo kabisa…muda mrefu kama wiki tatu…Hataki kutusalamia ameweka mgongo hivi. Tumeenda kumsalamia Baraka, ‘Baraka tumekuona, umependeza na tumekumiss’, lakini alikua hataki kuongea na sisi, alikua na chuki.
“Sasa mtu ambaye ana chuki, ana tatizo na wewe akitoa maoni kuhusu kitu chako unakua na mashaka kidogo kwamba ni honest opinion au kwasababu ya misunderstanding ambayo munayo. Na Baraka hii source ya kutuchukia mimi na Jux sababu tulimpunguza kwenye umoja ambayo tulikua tumeuanzisha kufanya shows, kufanya tours…tulimpunguza. Hatukuwai kusema, hatukuwai kumuaibisha kwenye media kusema kwamba tumempunguza au nini… Ni mdogo wetu tumesema tumlindie heshima, tumempunguza lakini hatutasema hivyo kwenye redio au kwenye mtendao…kwenye sehemu yoyote. Lakini kumbe yeye alikua na kinyongo, kwanzia hapo ukimtumia post, ukimwambia kitu akusaidie kushare anakuwekea hivi ‘hapana, no’, si support’. Kwa hivyo twasema kwamba ana chuki. Na kumpunguza ilikua lazima tumpunguze kwasababu ya discipline, kukosa nidhamu. Ilikua lazima tumpunguze.” Ben Pol alisema.

No comments