Christian Bella afunguka kuhusu chanzo cha yeye kulazwa ghafla nchini Congo
Baada ya wiki iliyopita kusambaa picha mitandaoni za muimbaji Christian Bella zikimuonyesha akiwa amelazwa hospitali nchini Congo na kuzua hofu kwa mashabiki wa muziki wake, muimbaji huyo amefunguka kuzungumzia kitu ambacho kilimsibu.
“Namshukuru Mungu anaendelea vizuri, nililazwa kwa muda mfupi kutokana na uchovu lakini baada ya kufanyiwa vipimo nilikutwa nimechoka tu. Kwahiyo baada ya kupumzika niliruhusiwa lakini niliambiwa natakiwa nitenge muda wa kumpumzika kwa sababu nilikuwa na tour ya muda mrefu kwa hiyo mwili ulikuwa umechoka sana,” alisema Bella.
Muimbaji huyo ambaye ni raia wa Congo, kwa sasa amerejea nchini Tanzania kwaajili ya kuendelea na shughuli zake za muziki baada ya kuwa na tour kubwa ya nchi mbalimbali za Afrika Mashariki na Kati
No comments