Breaking News

BURUDANI: Japo nimeachana na Nandy ila bado…. – Mc Pilipili

Mchekeshaji wa Tanzania, Emmanuel Mathias(Mc Pilipili) amefunguka juu ya mahusiano aliyokuwa nayo na mkali wa ngoma ya’ One Day’ Nandy ambapo ameeleza kuwa japo waliachana bado wana mawasiliano mazuri .
Akiongea na Bongo5 hivi karibuni, Mc huyo ameeleza kuwa yeye msanii huyo wa bado wanamawasiliano mazuri tu, kwa kudhihirisha hilo ndiyo maana amekuwa shabiki wake katika muziki.
“Mimi na Nandy bado tuna wasiliana vizuri tu, nimerudi kutoka Marekani nimemletea zawadi ya Perfume, hata hivyo yeye yupo Kenya amenicheki kunijulisha kuwa yupo huko na ninaona picha anazopost akiwa huko, unajua mimi na Nandy tumeachana sio kwa ubaya, ila tulifanya hivyo kwa sababu Nandy alikuwa anataka afanye kazi zake kwa uhuru zaidi,” aliongea Mc Pilipili.
Ameongeza kuwa” Kuachana na Nandy hapakuwa na kosa, sikutaka kumpa stress (mawazo)ni makubaliano yetu yalikuwa ni hayo, sio kwa ubaya ni kwa wema kabisa. Sikutaka kuzima ndoto zake kwani ningeshindwa kuwa mume wake ningekuwa nimezima ndoto zake za kufika hapo alipo.”

No comments