Naija yaongoza kwa wasanii wanaoingiza pesa nyingi Afrika kwa mujibu wa Forbes wakifuatiwa na South Africa, Tanzania hatumo....
Jarida la Forbes Africa la mwezi May 2017 limeandaa list ya wasanii 10 wanaoingiza pesa nyingi zaidi Africa.
List hiyo ambayo inaongozwa na msanii wa Nigeria, Akon na
nafasi ya pili ikichukuliwa na producer na msanii wa Afrika Kusini,
Black Coffee imendaliwa kwa vigezo vya thamani ya endorsement
wanazozipata, umaarufu, viwango vya show zao wanazofanya, mauzo, tuzo,
watazamaji wao kwenye chaneli za YouTube, kutokea kwenye magazeti, kuwa
na ushawishi mkubwa kuliko wengine, uwekezaji na uwepo wao katika
mitandao ya kijamii.
1.AKON
Akon anaingia kwenye list hii kutokana na
mauzo ya albumu zake akribani milioni 35 zilizouzwa kila pande ya
dunia, kingine kikubwa ni kwamba Akon ameshajinyakulia grammy tano huku
akiwa ameingiza ngoma 45 katika chati za ya Billboard hot 100.
2. BLACK COFFEE, AFRIKA KUSINI
Maarufu sana kutokana na tuzo ambazo
amewahi kujishindia kama BET, wengi wanamfahamu kwa jina kamili
la Nkosinathi Maphumulo , kubwa zaidi Black Coffee, ameingia kwenye
albumu mpya ya Drake ‘More Life’ ambayo inafanya vizuri sokoni.
3. HUGH MASEKELA
Alizaliwa Witbank, Mashariki
mwa Johannesburg, Hugh Masekela ashafanya takriban albumu 43 ambazo zote
hizo aliwahi kuperforme na wasanii wakubwa kama Marvin Gaye, Stive
Wonder, Miriam Makeba na wengine kibao.
4. DON JAZZY, NIGERIA
Ni msanii pia ni producer kutoka nchini
Nigeria ambaye amejibebea umaarufu kutokana na mafanikio makubwa katika
game ya muziki Afrika mpaka Marekani ambapo alifanikiwa kuja na label
yake ya Mavins ambayo nayo imebeba vichwa vingi vikubwa vinavyofanya
vizuri Afrika, Do Jazzy alianza tasnia ya muziki tangu yuko mdogo
kanisani mpaka kufikia hatua hii aliyokuwa nayo sasa. Pia msanii kutoka
kwenye label yake ya Mavins, Tiwa Savage alisaini katika label ya Jay Z,
Roc Nation.
5. TINASHE, ZIMBABWEAN-AMERICAN
Maarufu na ngoma kama ya “2 On
aliyomshirikisha School Boy” pamoja na “How long” ya Davido, Tinashe ni
mchanganyiko Mzimbwabwe pamoja na America, vilevile ni mwandishi mzuri
wa nyimbo, muimbaji, muigizaji pamoja na dancer. Alishashinda tuzo kibao
kupitia wimbo wake wa “2 On”. Tinashe aliingia kwenye listi ya kuwa
mwanamke wa kwanza kutokea katika jarida la Play Boy bila kukaa utupu.
6. JIDENNA, NIGERIAN-AMERICAN
Mzee wa Classic, anajulikana kama Jidenna
Theodore Mobisson, mbali na kuwa maarufu katika tasnia ya muziki,
Jiddena angekuwa ni moja ya masound Engineer, amejizolea umaarufu na
ngoma yake ya Classic Man, Yoga, Long Live Chief na zingine kibao.
7. WIZKID, NIGERIA
Moja ya wasanii wa Afrika wanaofanya
vizuri duniani na kugusa kila mioyo ya wapenda muziki, ameingia kwenye
tuzo nyingi kubwa duniani kupitia wimbo wa “One Dance” alioshirikishwa
na Drake pamoja na “Come Closer” anayotamba nayo kwa sasa.
8. DAVIDO, NIGERIA
Ni mmoja kati ya wasanii ambao wamepigana
sana kufikia hatua ambayo yupo nayo sasa akiwa na ngoma nyingi kali na
kutengeneza njia kibao kwa muziki wa Afrika kuchomoza zaidi. Alishapiga
kolabo na msanii kutoka Bongo, Diamond platnumz.
9. SARKODIE, GHANA
Alianza kama underground rapper katika
tasnia ya muziki wa kiafrika mpaka kufikia hatua ya mghana wa kwanza
kushinda tuzo ya BET, maarufu na ngoma “No kissing Baby”, “Pain Killer”.
10. OLIVER MTUKUDZI, ZIMBABWE
Albumu 65 zikiwa kwenye tasnia yake ya
muziki, katika miaka yake 41 ya muziki, nyimbo zake zimekuwa zikichezwa
duniani kote, maarufu zaidi masikioni mwa mashabiki na kibao cha “Neria”
No comments