“Mimi simtaki Diamond tena!” Wema Sepetu amwambia shabiki wake Instagram
Japo ni wengi bado hutarajia Wema Sepetu na Diamond Platnumz kurudiana, mrembo huyu ameweka wazi kuwa hamtamani Diamond tena na mapenzi yao yalikwisha kitambo sana.
Wema Sepetu alisema haya baada ya mmoja wa mashabiki wake aliandika kumuuliza iwapo ameshindwa kumpata Diamond Platnumz kupitia Instagram. Shabiki huyo aliandika kusema,
"Wema Kwa uzuri huo umeshindwa kumkamata Diamond mpaka anakupa mawazo wanaume hawana lolote jitahidi"
Kupitia tu Instagram Wema pia yeye alimpa shahidi huyo jibu ambalo lilidhibitisha kuwa mrembo huyu ameyaacha maisha yake ya kitambo na hivi sasa anatarajia mwanaume ambaye atamchukua alivyo. Wema aliandika kusema,
@Veronikakihonga Sasa baby alokwambia mi namtaka Diamond ni nani…?Life has to go on… Yule ni baba wa watoto wawili Jamani… Its about time u guys accept that me and Naseeb are no more. Mnachotakiwa ni kuniombua ni nipate mwanaume Bora na sio Bora mwanaume…Mwenye heshima zake tena ambaye hata haijulikani…Kajisemea dada angu @mangekimambi…mwenye hela miiingi
No comments