Jackie Chan na Sylvester Stallone kuja na movie mpya
Baada ya kufanya vizuri na movie ya ‘The Expendables’, waigizaji wakongwe wa Filamu duniani, Sylvester Stallone na Jackie Chan, wametangaza ujio wa filamu yao mpya ya Action waliyoipa jina la Ex Baghdad.
Filamu hiyo ya Ex-Baghdad ambayo haijatangazwa tarehe ya kutoka, itaongozwa na mtayarishaji maarufu wa Filamu Duniani, Scott Waugh, ambaye alishawahi kutengeneza filamu kama 6 Below na Need for Speed .
Ex-Baghdad ni filamu ambayo itaelezea mkasa wa wanajeshi wawili wastaafu (Chan na Stallone) ambao wanatakiwa kulisindikiza kundi la raia kutoka eneo hatari la mji wa Baghdad kwenda mji mwingine salama wa Mosul .
Kwa mujibu wa mtandao wa Deadline gharama za utengenezaji wa Filamu hiyo unakadiliwa kutagharimu kiasi cha Dola Milioni 80 za kimarekani hadi kukamilika.
Jack Chain na Sylvester Rambo walishawahi kuingiza kwa pamoja kwenye ‘The Expendables’ hivyo naamini ujio wao wa Movie hiyo ya Ex-Baghdad utakuwa ni moto wa kuotea mbali.
By Godfrey Mgall
No comments