Breaking News

Kazi aliyonipa Diamond nimeifanya – Q Chief

Msanii mkongwe wa muziki, Q Chief amesema amekamilisha ujio wa wimbo wake mpya wenye mahadhi ya Zouk













Muimbaji huyo amedai alishauriwa na Diamond Platnumz kufanya muziki wa Zouk kwa kuwa ni muziki ambao alikuwa anaufanya katika kipindi cha nyuma na kumpatia mafanikio makubwa.

Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Q Chief amedai wimbo huyo ambao umetayarishwa na maproducer watatu, utawarudisha nyuma wale mashabiki wa muziki wake ambao waliumiss muziki huo.

“Namshukuru Mungu kazi imekamilika na mara mwisho kuzungumza na Diamond aniambia anamtaka yule Q Chief wa zamani, yule ambaye alikuwa anaimba Zouk,” alisema Q Chief. “Kazi imekamilika bado maproducer kumalizia kazi zao, Diamond aliniambia nifanye Zouk na kweli nimefanya,”

Pia alisema wimbo huo alikuwa amshirikishe Diamond lakini baada ya watu wake wa karibu kuusikiliza nakumshauri autoe akiwa mwenyewe.

Muimbaji huyo kwa sasa anafanya maandalizi ya show yake ya ‘Miaka 15 ya Qchief’ itayofanyika April 30 katika ukumbi wa Next Door Masaki jijini Dar es salaam.

Chanzo: Bongo 5

No comments