Breaking News

Barabara za rami kukuza sekta ya utalii Mara




Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt Charles  Mlingwa  akiongea na waandishi  wa habari baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Makutanto Juu- Sanzate hivi karibuni



Mlingwa akiongea na Waandishi wa Habari


Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt Charles Mlingwa  hivi karibuni amekagua miradi mikubwa ya kitaifa ya barabara ukiwemo  ujenzi wa barabara ya Makutano Juu- Sanzate ambayo inajengwa kwa kiwango cha rami na kusema kukamilika kwa barabara  ni muhimu kwa maendeleo ya  sekta ya utalii katika Mkoa wa Mara.Mbali kurahisisha usafiri kwa wakazi wa Wilaya za Butiama, Serengeti na Bunda , barabara hiyo itaunganisha Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Ziwa Victoria na hivyo kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea Mkoa wa Mara. 

No comments