Atembezwa Nusu UCHI Na Kisha Kulazimishwa Kula Kinyesi kwa Kosa la Kumtukana Mama Yake
Wanawake
wa kijiji cha Kisungamile kilichopo katika Kata ya Matai wilayani
Kalambo katika mkoa wa Rukwa wamemwadhibu Vitus Nyami (26) kwa
kumtembeza nusu uchi na kulazimisha kula kinyesi cha ng’ombe kwa kosa la
kumtukana mama yake mzazi matusi ya nguoni.
Aidha
wanawake hao walitumia mfuko wa ‘salphate’ kufunika sehemu za siri za
kijana huyo kisha wakaanza kumtembeza mitaani kijijini humo huku
wakiimba nyimbo za kabila la Kifipa wakilaani tabia ya kijana huyo ya
kumtukana mama yake mzazi matusi ya nguoni kila kukicha .
Walidai
kukasirishwa na tabia ya kijana huyo wa kiume kumtukana mzazi wake wa
kike matusi ya nguoni, hivyo walilazimika kumfunga kamba na kumtembeza
mitaani kijijini humo akiwa nusu uchi.
Mwenyekiti
wa kijiji cha Kisungamile, Didas Musa alikiri kutokea kwa mkasa huo
juzi ambapo mtuhumiwa huyo alitembezwa mitaani kwa saa sita kuanzia saa
1:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana.
Akifafanua
alisema kuwa licha ya adhabu hiyo ya kutembezwa nusu uchi mitaani na
kucharazwa viboko 15, pia ameamriwa kulipa mbuzi mmoja, unga wa sembe
debe moja na mafuta ya kupikia lita moja.
“Adhabu hii kwa kijana hutolewa na akina mama ambapo mimi kama kiongozi kazi yangu ni kuibariki tu,”
alisisitiza . Mkazi wa kijiji hicho, Obedi Mwanakatwe alisema kijana
huyo amekuwa akimtukana mama yake mara kwa mara , tabia ambayo imekuwa
ikiwachukiza akinamama kijijini humo ambapo waliandamana na kumkamata
kijana huyo .
“Baada
ya akinamama hao wenye hasiri kumkamata kijana huyo walimpeleka kwenye
shimo lililojaa kinyesi cha ng’ombe kisha wakampaka kinyesi hicho mwili
mzima wakiwa wamechanganya na unga wakisaidiwa na wanaume, walimtembeza
uchi kijana huyo mitaani kijijini humo,” alieleza.
Stela
Tenganamba alisema baada ya kumtembeza kwa muda mrefu waliamua kumlisha
kinyesi cha ng’ombe na kumpaka mwili mzima sambamba na kumroweka kwenye
matope.
Adhabu
hiyo iliwekwa enzi za mababu zao , ambapo mtu yeyote anayetukana matusi
hadharani huchukuliwa hatua hiyo sambamba na kulipishwa ng’ombe mmoja,
mbuzi, unga debe moja na mafuta ya kupikia lita moja.
Akifafanua
alisema kuwa baada ya kutembezwa mitaani akiwa uchi hupelekwa kwa
Mwenyekiti wa Kijiji ambaye hutoa adhabu kulingana na akinamama
watavyoona inafaa
No comments