Polisi wathibitisha wanafunzi 31 kufariki katika ajali Arusha
Ajali mbaya imetokea Karatu Arusha katika mlima Rhotia baada ya basi aina ya Coaster lililokuwa limebeba wanafunzi kutumbukia kwenye korongo na kusadikiwa kusababisha vifo kwa wanafunzi kadhaa.


Taarifa za awali zinasema kuwa wanafunzi hao walikuwa wanakwenda kufanya mazoezi ya ujirani mwema Karatu.
Kamanda wa Polisi, mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema wanafunzi 31 na walimu wao wamefariki katika ajali iliyotokea wilayani Karatu, ulipo mto Mlera.
Mkumbo ambaye yupo njiani akielekea wilayani Karatu amesema wanafunzi waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni wa shule ya mchepuo wa Kiingereza, iitwayo LackVicent ya mjini Arusha.
Pole sana kwa ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza watu wao katika ajali hii mbaya, Mungu azilaze pema roho zao.


Source:Mwananchi
No comments